Kuhusu Programu ya ENGINE


ENGINE (Programu ya kuwezesha ukuaji kupitia uwekezaji na biashara) ni programu ya miaka minne inayofadhiliwa kupitia "Feed the Future " na USAID. Inatekelezwa na IESC kupitia "Volunteers for Economic Growth Alliance (VEGA) ". Programu hii inataka kuhuisha sekta za udhibiti, habari, na fedha zinazohamasisha uwekezaji wa ndani na nje kwenye mikoa ya kusini inayojihusisha na kilimo ya Mbeya, Iringa,na Morogoro, pamoja na Zanzibar.


Programu inalenga kwenye ngazi ya wilaya, kwa kutumia mbinu ya kufanya kazi na mamlaka za serikari za mitaa, sekta binafsi, washauri wa biashara, taasisi za fedha, na wajasiriamali. Shughuli za programu zimegawanywa katika sehemu tatu:


  1. Kutekeleza sera kwa ajili ukuaji. Kuongeza uwezo wa sekta binafsi kuzungumza na serikali kwa ufanisi kuweka ajenda ya sera na kuboresha uwezo wa sekta binafsi kutekeleza sera.
  2. Kuwezesha ukuaji wa biashara. Kuimarisha uwezo wa biashara (SME) na kujenga uhitaji wa huduma za washauri wa biashara wakati ikisaidia kampuni zinazotoa huduma za ushauri wa biashara kuwa endelevu.
  3. Upatikanaji wa fedha kwa ajili ya ukuaji. Kupanua upatikanaji wa fedha kwa wafanyabiashara ndogo ndogo (SMEs), hasa wajasiriamali wanawake na vijana, kuwezesha ongezeko la uwekezaji na ukuaji.


" Feed the Future " ni mpango toka serikali ya Marekani kudhibiti njaa duniani. Ikiwalenga wakulima wadogo wadogo, hasa wanawake, " Feed the Future " inasaidia nchi washirika kuendeleza sekta za kilimo ili kuchochea ukuaji wa kiuchumi na biashara kuongeza kipato na kupunguza njaa, umasikini na utapiamlo. USAID ni wakala wa serikali ya Marekani anayeongoza kufanya azi ya kukomesha umasikini uliokithiri duniani na kuwezesha ustahimilivu na demokrasia katika jamii ili zitambue uwezo wao.