Kuhusu Bizfundi

Bizfundi ni jukwaa la biashara lililoanzishwa na program ya “ENGINE” inayofadhiliwa na USAID , kutokana na utambuzi wa uhitaji wa habari miongoni mwa wamiliki wa biashara ndogo ndogo ndani ya Tanzania – hasa zinazohusiana na huduma za ushauri/utaalamu wa biashara na upatikanaji wa fedha.

Tovuti ya Bizfundi na toleo mbadala kwenye App ya simu ya android, zimebuniwa kuwezesha wamiliki wa biashara kutambua, kutathmini na kuwasiliana kwa haraka na washauri na makampuni mbalimbali yanayotoa huduma za kimkakati na utendaji kwa biashara (wanajulikana kama washauri wa biashara)

Wamiliki wa biashara wanawezeshwa kutafuta washauri wa biashara kwa kutumia aina za huduma wanazotoa , au sehemu walipo. Vilevile, washauri wa biashara wanawezeshwa kutafuta wafanya biashara na kuchuja ili kutangaza huduma zao kwa ubora zaidi. Toleo jipya la jukwaa hili litajumuisha uunganishaji kwenye taasisi za fedha.

Jukwaa la Bizfundi lipo kwenye matengenezo. Matoleo ya ziada na uboreshaji wa muonekano vitafanyika mara kwa mara. Maoni na ushauri yanaruhusiwa. Jisikie huru kuwasiliana nasi.