Warning: file_get_contents(https://geoip-db.com/json): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 502 Bad Gateway in /home/bizfundi/public_html/digitalPlatform/mainHeader.php on line 25

Warning: Cannot modify header information - headers already sent by (output started at /home/bizfundi/public_html/digitalPlatform/mainHeader.php:25) in /home/bizfundi/public_html/digitalPlatform/mainHeader.php on line 46
Bizfundi - Mfumo wa Dijitali

Bizfundi ni jukwaa la biashara lililoanzishwa na program ya “ENGINE” inayofadhiliwa na USAID , kutokana na utambuzi wa uhitaji wa habari miongoni mwa wamiliki wa biashara ndogo ndogo ndani ya Tanzania – hasa zinazohusiana na huduma za ushauri/utaalamu wa biashara na upatikanaji wa fedha.

Tovuti ya Bizfundi na toleo mbadala kwenye App ya simu ya android, zimebuniwa kuwezesha wamiliki wa biashara kutambua, kutathmini na kuwasiliana kwa haraka na washauri na makampuni mbalimbali yanayotoa huduma za kimkakati na utendaji kwa biashara (wanajulikana kama washauri wa biashara)

Wamiliki wa biashara wanawezeshwa kutafuta washauri wa biashara kwa kutumia aina za huduma wanazotoa , au sehemu walipo. Vilevile, washauri wa biashara wanawezeshwa kutafuta wafanya biashara na kuchuja ili kutangaza huduma zao kwa ubora zaidi. Toleo jipya la jukwaa hili litajumuisha uunganishaji kwenye taasisi za fedha.

Jukwaa la Bizfundi lipo kwenye matengenezo. Matoleo ya ziada na uboreshaji wa muonekano vitafanyika mara kwa mara. Maoni na ushauri yanaruhusiwa. Jisikie huru kuwasiliana nasi.  1. Wanatoa maono ya fursa mpya za biashara
  2. Wanaongeza uwezo wako na hulka kwenye kutambua matatizo ya biashara, kufanya maamuzi, na kumiliki mpango wa utekelezaji wa biashara
  3. Wanaboresha ufanisi wa utendaji na kuongeza mtandao wako kupitia muongozo na ushauri juu ya ujuzi wa kuendesha biashara yenye mafanikio
  4. Ukuaji wa biashara kutokana na usimazi wa biashara ulioboreshwa na ujuzi wa biashara kupitia mafunzo kama ya ujuzi wa masoko, ujuzi wa usimamizi wa fedha, ujuzi wa kutengeneza mpango biashara n.k
  5. Uwezo na mbinu za kukaribia huduma za fedha kutokana na mafunzo ya utayari wa kupokea mikopo kabla ya kwenda kwenye taasisi za fedha
  6. Ukuaji na uendelevu wa biashara kutokana na kutumia teknolojia mpya ambayo inaongeza ufanisi wa biashara, ukuaji, na uendelevu
  7. Kuongeza upatikanaji wa masoko kutokana na mahusiano yanayokuza na kuwezesha ongezeko la wauzaji na wanunuzi na maendeleo ya biashara yanayohusisha ushirikiano kati ya kampuni za ndani na nje
Pakua App ya Bizfundi
Tembelea MSME information Portal ya TPSF
Habari kutoka MSMEs information Portal
Habari za Biashara Tanzania